Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 5:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Basi, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapokuja. Tazameni mkulima anavyongoja kwa subira mimea yake itoe mavuno ya thamani. Yeye hungojea kwa subira mvua za masika na za vuli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana Isa. Tazameni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani, na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua ya kwanza na ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana Isa. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua za kwanza na za mwisho.

Tazama sura Nakili




Yakobo 5:7
32 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.


Kwa sababu hii na ninyi mwe tayari; kwa sababu saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.


Walakini Mwana wa Adamu atakapokuja, je! ataiona imani duniani?


Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu kwa nguvu na utukufu mwingi.


Nazo penye udongo mwema, hawa ndio ambao kwamba kwa moyo mzuri na mwema hulisikia neno, wakalishika, wakazaa kwa saburi.


Yesu akamwambia, Nikitaka huyu akae hatta nijapo imekukhusu nini? wewe unifuate mimi.


Bassi neno hili lilienea katika ndugu kwamba mwanafunzi yule hafi: walakini Yesu hakumwambia, Hafi; bali, Nikitaka akae hatta nijapo imekukhusu nini?


Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


hatta hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;


Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la wema kwa njia ya imani.


Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.


mkiwezeshwa kwa nwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya killa namna na uvumilivu pamoja na furaha;


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.


Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.


Watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.


Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itakushuhudieni, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku hizi za mwisho.


na kusema, iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali hiyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo