Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 5:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Basi, ungamanieni dhambi zenu, na ombeaneni, ili mpate kuponywa. Sala ya mtu mwema ina nguvu ya kutenda mengi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kwa hiyo, ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu, tena yanafaa sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwa hiyo, ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana.

Tazama sura Nakili




Yakobo 5:16
68 Marejeleo ya Msalaba  

Na yo yote mtakayoyaomba katika kusali, mkiamini, mtapokea.


wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Wakamwendea inchi yote ya Yahudi, nao wa Yerusalemi, wakabatizwa nae katika mto Yardani, wakiziungama dhambi zao.


Wakaenda zao, wakazunguka katika vijiji, wakiikhubiri injili, na kuponya watu killa pahali.


Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi: bali mtu akiwa mcha Mungu, na kufanya mapenzi yake, huyo amsikia.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.


Simon akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Mungu, yasinifikilie mambo haya uliyosema.


kama ilivyoandikwa, ya kama, Hakuna mwenye haki hatta mmoja.


Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wote waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwake mtu mmoja watu wote wameingizwa katika hali ya wenye haki.


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


Kwa imani Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kain; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena.


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


mkaifanyia miguu yenu njia za kunyoka, illi kitu kilicho kilema kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.


Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.


yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.


na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo