Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 5:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Tunawaita hao wenye heri kwa sababu walivumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wa Yobu, na mnajua jinsi Bwana alivyomtendea mwishoni. Maana Bwana amejaa huruma na rehema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kama mnavyojua, tunawahesabu wale waliovumilia kuwa wabarikiwa. Mmesikia habari za uvumilivu wake Ayubu, na mmeona kile ambacho hatimaye Mwenyezi Mungu alimtendea. Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma, na amejaa rehema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kama mnavyojua, tunawahesabu kuwa wabarikiwa wale waliovumilia. Mmesikia habari za uvumilivu wake Ayubu na mmeona kile ambacho hatimaye Mwenyezi Mungu alimtendea. Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma, na amejaa rehema.

Tazama sura Nakili




Yakobo 5:11
53 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Na rehema zake vizazi hatta vizazi Kwao wanaomcha.


Kwa sababu killa aombae hupewa: nae atafutae hupata: nae abishae hufunguliwa.


Bassi mwe na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa:


Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba?


illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:


Lakini Mungu kwa kuwa mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda,


Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;


Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, mwe na kiasi, kwa utimilifu mkiitumainia ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.


Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike;


Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo