Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 4:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nyinyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ninyi wanaume na wanawake wazinzi, hamjui ya kwamba urafiki na dunia ni uadui na Mwenyezi Mungu? Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Yakobo 4:4
24 Marejeleo ya Msalaba  

Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara, wala hakitapewa ishara, ilia ishara ya nabii Yunus.


Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya nabii Yunus. Akawaacha, akaenda zake.


Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.


Walakini wale adui zangu wasiotaka niwatawale, waleteni huku mkawachinje mhele zangu.


Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeyapenda yaliyo yake: lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua ninyi katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.


Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu uliwachukia, kwa kuwa wao si watu wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.


Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.


Kwa maana tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.


Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sharia ya Mungu wala haiwezi.


Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja wa dunia bii? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia liii kuwa upumbavu?


Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upumbavu wa lile neno linalokhubiriwa.


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo