Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yakobo 4:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, illi mvilumie kwa tamaa zenu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mpate kuvitumia hivyo mtakavyopata kwa tamaa zenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya, ili mpate kuvitumia hivyo mtakavyopata kwa tamaa zenu.

Tazama sura Nakili

Yakobo 4:3
25 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomha. Mwaweza kuuywea kikombe nitakachonywea mimi, na kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? Wakamwambia, Twaweza.

Yesu akawaambia, Hamjui mnaioliomba. Mnaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, na kubatizwa nbatizo nibatizwao mimi?

Kwa sababu killa aombae hupewa: nae atafutae hupata: nae abishae hufunguliwa.

Hatta baada ya siku si nyingi yule mdogo akakusanya vitu vyake vyote, akasafiri kwenda inchi ya mbali: akatapanya huko mali zake kwa maisha ya uasharati.

Bali alipokuja mwana wako huyo, aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.

VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?

na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia:

Tufuate:

Matangazo

Matangazo