Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 4:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Mtoa sharia na mbukumu ni mmoja tu, awezae kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umbukumuye mwenzako?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Yuko Mtoa sheria mmoja tu na yeye peke yake ndiye Hakimu; ndiye awezaye kuokoa au kuangamiza. Lakini wewe ni nani hata umhukumu jirani yako?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Yuko Mtoa sheria mmoja tu na yeye peke yake ndiye Hakimu, ndiye awezaye kuokoa au kuangamiza. Lakini wewe ni nani hata umhukumu jirani yako?

Tazama sura Nakili




Yakobo 4:12
11 Marejeleo ya Msalaba  

Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.


Illa nitawaonya mtakaemwogopa: Mwogopeni yule aliye na uweza baada ya kuua mtu kumtupa katika Jehannum: naam, nawaambieni, Mwogopeni yule.


Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha.


Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha.


KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.


La! si hivyo, ee bin-Adamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Ya nini nkanifanza hivi?


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo