Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 4:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Ndugu, msilaumiane nyinyi kwa nyinyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu sheria. Kama ukiihukumu sheria, basi, wewe huitii sheria, bali waihukumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu yeyote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu, anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria, bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ndugu, msineneane mabaya ninyi kwa ninyi. Mtu yeyote anayesema mabaya dhidi ya ndugu yake au kumhukumu anasema dhidi ya sheria na kuihukumu. Unapoihukumu sheria, basi huishiki sheria bali umekuwa hakimu wa kuihukumu hiyo sheria.

Tazama sura Nakili




Yakobo 4:11
24 Marejeleo ya Msalaba  

msipatilize, nanyi hamtapatilizwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.


KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.


Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki.


Tusemeje, bassi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalijua dhambi illa kwa sharia: kwa maana singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


Uchungu wote na hasira na ghadhabu na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na killa ubaya;


Vivi hivi wanawake wawe watu wa utaratibu, si wasingiziaji, watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.


wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,


Na wazee wa kike vivyo hivyo wawe na mwenendo wa utakatifu, wasiwe wasiugiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;


Msidanganyike, ndugu zangu wapenzi.


Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu;


Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake.


Illakini mkiitimiza sharia ya kifalme kama ilivyoandikwa. Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vyema.


Watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.


Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.


Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


BASSI, mkiwekea mbali uovu wote na hila yote na unafiki na husuda na niasingizio yote,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo