Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 4:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mapigano na ugomvi wote kati yenu vinatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mapigano na ugomvi wote kati yenu vinatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mapigano na ugomvi wote kati yenu vinatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ni kitu gani kinachosababisha mapigano na ugomvi miongoni mwenu? Je, haya hayatokani na tamaa zenu zinazoshindana ndani yenu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ni kitu gani kinachosababisha mapigano na ugomvi miongoni mwenu? Je, haya hayatokani na tamaa zenu zinazoshindana ndani yenu?

Tazama sura Nakili




Yakobo 4:1
24 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, mauaji, mazini, asharati, uizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano;


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


lakini katika viungo vyangu naona sharia nyingine inapiga vita na ile sharia ya akili zangu, na kunifanya mateka va ile sharia ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.


Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao.


Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sharia ya Mungu wala haiwezi.


Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana liizi zimepingana, hatta hamwezi kufanya nmayotaka.


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi:


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Maswali ya upuzi, na vitabu vya nasaba, na magomvi, na mashindano ya sharia, ujiepushe nayo. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.


Lakini killa mmoja hujaribiwa akivutwa na kudanganywa na tamaa yake mwenyewe.


Mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, illi mvilumie kwa tamaa zenu.


Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza, za ujinga wenu;


Mapenzi, nakusihini kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho;


wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:


Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo