Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 3:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Kaangalieni jinsi moto mdogo uwasbavyo kuni nyingi sana. Nao ulimi ni moto, ulimwengu wa uovu. Ndio khabari ya ulimi katika viungo vyetu, huutia najis mwili wote, huliwasha moto gurudumu la maumbile, nao huwashwa moto na jehannum.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa Jehanamu.

Tazama sura Nakili




Yakobo 3:6
62 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo.


Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.


Hapana kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia najis, bali vimtokayo, ndivyo vimtiavyo najis yule mtu.


Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu.


tena katika baadhi yenu wataondoka watu, wakisema mapotofu, wawavute wanafunzi kwenda nyuma yao.


Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja?


Wakasimamisha mashahidi wa uwongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati:


ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hawo wanapindua uyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.


Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?


Maana killa aina ya nyama, na ya ndege, na ya nyama watambaao, na ya vitu vilivyo baharini vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wana Adamu.


Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,


Kwa hiyo, nikija, nitamkumbusha matendo yake ate-ndayo, akitoa upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, yeye mwenyewe hawakaribishi ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi.


wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo