Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 3:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Hekima hii siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na ya Shetani,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Hekima kama hiyo haishuki kutoka mbinguni, bali ni ya kidunia, isiyo ya kiroho, na ya kishetani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Hekima ya namna hiyo haishuki kutoka mbinguni, bali ni ya kidunia, isiyo ya kiroho, na ya kishetani.

Tazama sura Nakili




Yakobo 3:15
30 Marejeleo ya Msalaba  

Yule bwana akamsifu wakili asiye haki, kwa kuwa alitenda kwa busara: kwa maana wana wa zamani hizi wana busara kuliko wana wa nuru, katika kizazi chao wenyewe.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?


wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika,


bali Mungu aliyachagua mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena alivichagua vitu dhaifu vya dunia illi wenye nguvu waaibishwe;


Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.


Maana hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasae wenye hekima katika hila yao.


Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo.


mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.


ambae kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kazi kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za nwongo,


ROHO yanena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho watu watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani,


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa.


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


Watu hawo ndio wajitengao, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Lakini nawaambia ninyi, nao wengine walio katika Thuatera, wo wote wasio na mafundisho haya, wasiozijua fumbo za Shetani kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yen umzigo mwungine.


Na juu yao wana mfalme, malaika wa abuso, jina lake kwa Kiebrania Abaddon, na kwa Kiyunani jina lake Apollion.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo