Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 3:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na magomvi mioyoni mwenu msijisifu, wala msiseme nwongo juu ya kweli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Lakini ikiwa mna wivu na ni wenye chuki na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu kwa ajili ya hayo wala msiikatae kweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Lakini ikiwa mna wivu na ni wenye chuki na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu kwa ajili ya hayo wala msiikatae kweli.

Tazama sura Nakili




Yakobo 3:14
42 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda.


Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada.


Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti;


Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu,


Wale wazee wetu wakamwonea wivu Yusuf, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja nae,


wakijawa na udhalimu wa killa namna ya zina, na novu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na khadaa;


Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.


Lakini wewe, ukiwa unakwitwa Myahudi na kuitegemea torati, na kujisifu katika Mungu,


na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, hasira na ghadhabu;


Upendo husubiri, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni,


Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.


Nanyi minejivuna wala hamkusikitika illi aondolewe kati yenu yeye aliyetenda jambo hilo.


Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


Lakini mkiumana na kulana angalieni msije mkaangamizana.


ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi,


husuda, ulevi, ulafi, na yanayofanana na haya; juu ya haya nawaambieni mapema, kama nilivyokwisha kuwaambieni, watu watendao mambo ya jinsi hii hawatanrithi ufalme wa Mungu.


Tusijisifu burre, tukichokozana na kuhusudiana.


Kwa maana hatta wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sharia; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kujisifia miili yenu.


Wengine wanakhubiri khabari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina: na wengine kwa nia njema.


Msitende neno lo lote kwa kushindana na kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, killa mtu na amhesabu mwenziwe kuwa hora kuliko nafsi yake;


atakae watu wote waokolewe wakapate kujua sana yaliyo kweli.


amejivuna, nae hakufahamu neno lo lote, bali hali yake hali va ugonjwa, kwa khabari ya maswali na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya,


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


maana hapo palipo wivu na magomvi, ndipo palipo machafuko, na killa tendo la aibu.


Ndugu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali ya kweli, na mtu mwingine akamrejeza;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo