Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 3:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Nani aliye na hekima na fahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aioneshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aionyeshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.

Tazama sura Nakili




Yakobo 3:13
46 Marejeleo ya Msalaba  

Jitieni nira yangu, jifunzeni kwa mfano wangu; kwa kuwa mimi ni mpole na moyo wangu umenyenyekea: nanyi mtapata raha rohoni mwenu;


Mwambieni binti Sayuni, Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, amepanda punda, Na mwana punda, mtoto wa punda.


Wa kheri wenye upole: maana hawo watairithi inchi.


Bassi killa asikiae haya maneno yangu, na kuyafanya, nitamfananisha na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba vake juu ya mwamba:


Nasema haya nipate kuwatahayarisheni. Je! ndivyo hivyo, kwamba kwenu hakuna hatta mtu mmoja mwenye hekima, awezae kukata maneno ya ndugu zake?


NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;


Bassi waonyesheni mbele ya makanisa bayana ya upendo wenu, na ya kujisifu kwetu kwa ajili yenu.


upole, kiasi; juu ya mambo ya jinsi hii hapana sharia.


NDUGU, mtu ajapogbafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrudini mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako nsijaribiwe wewe mwenyewe.


Lakini killa mtu aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakuwa na sababu ya kujisifu kwa nafsi yake tu, wala si kwa kujilinganislia na mwenzake.


kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendano;


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,


Mtu asiudharau ujana wako, bali uwe mfano kwao waaminio, katika usemi, na katika mwenendo, na katika upendo, na katika imani, na katika utakatifu.


Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.


akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli,


wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.


Msiwe na tabia ya kupenda fedha: mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.


Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, kapokeeni kwa upole neno lililopandwa, liwezalo kuokoa roho zenu.


Lakini mtu atasema, Wewe una imani, nami nina matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo yako, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.


MSIWE waalimu wengi, ndugu zangu, mkijua ya kuwa tutapata hukumu kubwa zaidi.


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi mwe watakatifu katika mwenendo wenu wote;


mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


bali mtu wa moyoni asiyeonekana, katika jambo lisiloharibika; ni roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo