Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 2:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Lakini nyinyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamiza na kuwapeleka mahakamani?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Lakini nyinyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamiza na kuwapeleka mahakamani?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Lakini nyinyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamiza na kuwapeleka mahakamani?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini. Je, hao matajiri si ndio wanaowadhulumu na kuwaburuta mahakamani?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini. Je, hao matajiri si ndio wanaowadhulumu na kuwaburuta mahakamani?

Tazama sura Nakili




Yakobo 2:6
38 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu.


Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.


na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku,


Hatta Gallio alipokuwa Prokonsuli wa Akaya, Wayahudi wakamwendea Paolo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu,


Saul akaliharibu kanisa, akiingia killa nyumba, na kuwabarura wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.


Je! hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau Kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha wasio na kitu? Niwaambieni? niwasifu kwa haya? Siwasifu.


nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri, na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,


Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, uliozuiliwa nanyi kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa Sabaoth.


Mmemhukumu mwenye haki mkamwua: nae hashindani nanyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo