Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 2:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na kupokea ufalme aliowaahidia wale wanaompenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na kupokea ufalme aliowaahidia wale wanaompenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na kupokea ufalme aliowaahidia wale wanaompenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ndugu zangu, sikilizeni: Je, si Mungu huwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi ufalme aliowaahidi wale wanaompenda?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mwenyezi Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao?

Tazama sura Nakili




Yakobo 2:5
54 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


Wa kheri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote, fahamuni.


Ndivyo alivyo yeye ajiwekeae nafsi yake akiba wala hawi tajiri machoni pa Mungu.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Ikawa maskini akafa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa Ibrahimu. Akafa na yule tajiri, akazikwa.


Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kuwa ulipokea mema yako katika maisha yako, na Lazaro kadhalika mabaya; lakini sasa yeye yupo hapa anafarajiwa, nawe unanmizwa.


Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama alivyoniwekea Baba yangu;


Nae akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, M kheri ninyi mlio maskini: kwa sababu ufalme wa Mungu ni wemi.


Ni nani katika wakubwa amwammiye, au katika Mafarisayo?


Nae akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Kharran, akamwambia,


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, Wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.


Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, illi, neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao wengi mashukuru yazidishwe, Mungu akatukuzwe.


kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.


ndio ishara ya hukumu ya haki ya Mungu illi mstabilishwe kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa;


watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo,


Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele.


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mwingi kuliko hazina za Misri.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Msidanganyike, ndugu zangu wapenzi.


Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu;


Lakini ndugu asiye na cheo afurahi kwa kuwa ametukuzwa;


tupate urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu,


Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuuingia ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.


Yeye ashindae atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, nae atakuwa Mwana wangu.


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo