Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 2:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vyema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani wanaamini hivyo na kutetemeka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.

Tazama sura Nakili




Yakobo 2:19
31 Marejeleo ya Msalaba  

Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla?


akinena, Tʼuna nini nawe, Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu.


Yesu akamjibu, Katika amri zote ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;


akalia kwa sauti kuu akanena, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, uniapie kwa Mungu kwamba hutaniadhibu.


Akawaambia, Mwaikataa vema amri ya Mungu mpate kushika hadithi zenu.


Ah, tuna nini nawe Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Akamfuata Paolo na sisi, akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kutukhubiri njia ya wokofu.


Yule pepo akawajibu, Yesu namjua na Paolo namfahamu, bali ninyi ni nani?


Na Paolo alipokuwa akitoa hoja zake katika khabari ya haki na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya khofu akajihu, Sasa enenda zako, nami nikipata wasaa nitakuita tena.


kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo.


Bassi, kwa khabari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hapana Mungu mwingine illa mmoja tu.


illakini kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu, aliye Baba, ambae vitu vyote vimetokana nae, na sisi twarejea kwake; na yuko Bwana mmoja Yesu Kristo, ambae kwa sabiki yake vitu vyote vimekuwa, na sisi kwa sabiki yake.


Aliye mjumbe si mjumbe wa mmoja; bali Mungu ni mmoja.


Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wana Adamu ni mmoja, mwana Adamu, Kristo Yesu,


Illakini mkiitimiza sharia ya kifalme kama ilivyoandikwa. Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vyema.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo