Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 2:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NDUGU zangu, msiwe na imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana mwenye utukufu, kwa kupendelea watu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwabague watu kamwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwabague watu kamwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwabague watu kamwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ndugu zangu, waumini katika imani ya Bwana wetu wa utukufu, Isa Al-Masihi, hawapaswi kuwa na upendeleo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ndugu zangu, kama waaminio katika imani ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, Bwana wa utukufu, msiwe na upendeleo kwa watu.

Tazama sura Nakili




Yakobo 2:1
29 Marejeleo ya Msalaba  

Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu.


Petro akafumhua kiuywa chake, akasema, Hakika nimekwisha kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;


nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Baada ya siku kadha wa kadha, Feliki akafika pamoja na Drusilla mkewe aliyekuwa Myahudi, akamwita Paolo akamsikiliza khabari za imani ya Kristo.


Nae akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Kharran, akamwambia,


kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapeni karama ya rohoni, illi mfanywe imara;


ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;


tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;


nwe mwenye imani na dhamiri njema; wengine wamezisukumia mbali hizo, wakavunja chombo cha imani.


Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.


PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa,


tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Msidanganyike, ndugu zangu wapenzi.


Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu;


nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri, na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu,


Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sharia kama wakosaji.


Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole,, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina wala unafiki;


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Watu hawa ni wenye kunungʼunika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno ya kiburi makuu mno, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.


Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo