Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 1:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Acheni saburi ikamilishe kazi yake, ili mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote.

Tazama sura Nakili




Yakobo 1:4
26 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Yule kijima akamwambia, Haya yote nimeyashika tangu utoto wangu: nimepmigukiwa nini tena?


Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.


Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.


Kwa subira yenu mtazipata robo zenu.


Nazo penye udongo mwema, hawa ndio ambao kwamba kwa moyo mzuri na mwema hulisikia neno, wakalishika, wakazaa kwa saburi.


mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.


Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;


Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


illi mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa illi atende killa tendo jema.


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa.


Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezae kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Maana yeye asiyekuwa na haya ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo