Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 1:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Lakini yeye anayeangalia kwa makini katika sheria kamilifu iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau, bali akatenda alichosikia, basi atabarikiwa katika kile anachofanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Lakini yeye anayeangalia kwa bidii katika sheria kamilifu, ile iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosikia, bali akalitenda, atabarikiwa katika kile anachofanya.

Tazama sura Nakili




Yakobo 1:25
41 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini yeye akasema, Bali afadhali wa kheri wenye kulisikia neno la Mungu na kulishika.


Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda.


Bassi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.


Sunagogi lilipofumukana, Wayahudi wengi na waongofu watawa wakashikamana na Paolo na Barnaba; nao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.


Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.


Bassi nikiisha kuupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hatta leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno illa yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa;


Fahamu, bassi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka ukali, bali kwako wema, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.


Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki.


Bassi torati ni takatifu na ile amri takatifu ua ya haki na wema.


Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa uletao khofu, hali mlipokea roho ya kufanywa waua, kwa hiyo twalia, Abba, Baba.


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


Jijaribuni nafsi zenu kwamba m katika imani; jithubutisheni nafsi zenu. Au bamjijui nafsi zenu, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu isipokuwa mmekataliwa?


bali kwa ajili ya ndugu za uwongo walioingizwa kwa siri.


KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.


Mchukuliane mizigo mkaitimize hivyo sharia ya Kristo.


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Lakini ataokolewa, kwa ule uzazi, kama wakidumu katika imani na npendo na utakatifu pamoja na moyo wa kiasi.


Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao.


mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo.


Semeni ninyi, katendeni kama watu watakaohukumiwa kwa sharia ya uhuru.


kama huru, na wasiontumia uhuru kwa kusetiri ubaya, bali kaina watumwa wa Mungu.


Bassi, na yakae ndani yenu maneno yale mliyoyasikia tangu mwanzo. Neno lile mlilolisikia tangu mwanzo likikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.


Wa kheri wazifuazo nguo zao, wawe na amri kuuendea mti wa uzima, na kuuingia mji kwa milango yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo