Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 1:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili, atapewa tuzo la uhai ambalo Mungu aliwaahidi wale wanaompenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili, atapewa tuzo la uhai ambalo Mungu aliwaahidi wale wanaompenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili, atapewa tuzo la uhai ambalo Mungu aliwaahidi wale wanaompenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji lile la uzima Mungu alilowaahidia wale wanaompenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mwenyezi Mungu alilowaahidia wale wampendao.

Tazama sura Nakili




Yakobo 1:12
49 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu.


na kazi ya uvumilivu uthabiti wa moyo, na kazi ya uthabiti wa moyo tumaini,


Na twajua ya kuwa mambo yote hushiriki kazi moja, ndio kuwapatia mema wale wampendao Mungu, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.


lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, Wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu, Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.


Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejuliwa nae.


Na killa ashindanae hujiweza katika yote: bassi hao kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi isiyoharibika.


Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiyetahayarishwa, ukitumia kwa halali neno la Mungu.


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;


Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaak, awe dhabihu; na yeye aliyezipokea ahadi alikuwa akimtoa mwana wake, mzaliwa wake wa pekee;


tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama na wana. Mwanangu, usikudharau kurudi kwake Bwana, Wala, usizimie ukikemewa nae;


Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.


Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Angalieni, twawaita wenye kheri wao waliovumilia. Mmesikia khabari ya uvumilivu wa Ayub, mmenona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwenye rehema nyingi, mwenye huruma.


Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike;


lakini kama mnavyoyashiriki mateso va Kristo furahini; illi na katika ufimuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe.


Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Na mchungaji mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka.


Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo