Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yakobo 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salamu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salamu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia nyinyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salamu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Isa Al-Masihi. Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni. Salamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Yakobo, mtumwa wa Mwenyezi Mungu na wa Bwana Isa Al-Masihi: Kwa makabila kumi na mawili yaliyotawanyika ulimwenguni: Salamu.

Tazama sura Nakili




Yakobo 1:1
41 Marejeleo ya Msalaba  

Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo;


Huyu si mwana wa sermala? mama yake sio yeye aitwae Mariamu? Na ndugu zake Yakobo, na Yose, na Simon, na Yuda?


Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


na Andrea, na Filipo, na Bartolomayo, na Mattayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Thaddayo na Simon Mkanani,


mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na kuketi katika viti vya enzi, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Mattayo na Tomaso, Yakobo wa Alfayo, na Simon aliyeitwa Zelote,


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani?


Hatta walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartolomayo na Mattayo, Yakobo wa Alfayo, na Simon Zelote, na Yuda wa Yakobo.


Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.


Na bao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akinena, Ndugu zangu, nisikilizeni,


Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wakhubirio mambo yake; katika killa mji husomwa killa siku katika masunagogi.


Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.


Na walikuwako Yerusalemi Wayahudi wakikaa, watu watawa, watu wa killa taifa chini ya uwingu.


Hatta siku ya pili yake Paolo akaingia kwa Yakobo pamoja naswi, na wazee wote walikuwako.


Klaudio Lusia kwa liwali il aziz Feliki salamu!


ambayo kabila zetu thenashara wanataraja kuifikia, wakimkhudumu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, ee Mfalme.


NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


Lakini sikumwona mtume mwingine illa Yakobo ndugu yake Bwana.


kwa maana kabla hawajaja watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo, alikula pamoja na watu wa mataifa, illakini walipokuja akarudi nyuma akajitenga, akiwaogopa waliotahiriwa.


tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu;


Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi. Eubulo akusalimu, na Pudente, na Lino, na Klaudia, na ndugu wote pia.


PAOLO, mtumwa wa Mungu, mtume wa Yesu Kristo, illi ienee imani ya wateule wa Mungu, na ujuzi wa kweli iletayo utawa,


PETRO, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Mtawanyiko, wakaao bali ya wageni katika Ponto, Galatia, Kappadokia, Asia na Bithunia,


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika killa kabila ya wana wa Israeli, watu mia na arubaini na nne elfu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo