Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 9:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Tuseme nini, bassi? Ya kwamba watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; yaani ile haki iliyo ya imani;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Basi tuseme nini? Watu wa mataifa ambao hawakutafuta wafanywe waadilifu, wamejaliwa kuwa waadilifu, kwa njia ya imani,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Basi tuseme nini? Watu wa mataifa ambao hawakutafuta wafanywe waadilifu, wamejaliwa kuwa waadilifu, kwa njia ya imani,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Basi tuseme nini? Watu wa mataifa ambao hawakutafuta wafanywe waadilifu, wamejaliwa kuwa waadilifu, kwa njia ya imani,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Kwa hiyo tuseme nini? Kwamba watu wa Mataifa ambao hawakutafuta haki, wamepata haki ile iliyo kupitia kwa imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Kwa hiyo tuseme nini basi? Kwamba watu wa Mataifa ambao hawakutafuta haki, wamepata haki ile iliyo kwa njia ya imani.

Tazama sura Nakili




Waroma 9:30
28 Marejeleo ya Msalaba  

kwa maana kwa moyo watu huamini hatta kupata haki, na kwa kinywa hukiri hatta kupata wokofu.


Na Isaya ana ujasiri mwingi, anasema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia.


Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakaepanda mbinguni? (yaani ni kumleta Kristo chini,)


Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.)


Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema;


Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sharia bali kwa wema aliopata kwa imani.


Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa haki.


Bassi ukheri huu ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba Ibrahimu kwa ajili ya imani yake aliliesabiwa wema.


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Tuseme nini bassi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!


bali Israeli wakiifuata sharia ya haki hawakuifikilia ile sharia.


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


Na hivyo sharia imekuwa mwalimu wa kutuleta kwa Kristo, illi tufanyiziwe wema kwa imani.


Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa.


Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la wema kwa njia ya imani.


kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.


tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;


Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda wayapendayo mataifa, kuenenda katika uasharati, ua tamaa, na ulevi, ua karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo