Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 9:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Kwa maana naliomba mimi mwenyewe niharamishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 kwa ajili ya ndugu zangu walio wa taifa langu! Kama ingekuwa kwa faida yao, ningekuwa radhi kulaaniwa na kutengwa na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 kwa ajili ya ndugu zangu walio wa taifa langu! Kama ingekuwa kwa faida yao, ningekuwa radhi kulaaniwa na kutengwa na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 kwa ajili ya ndugu zangu walio wa taifa langu! Kama ingekuwa kwa faida yao, ningekuwa radhi kulaaniwa na kutengwa na Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Al-Masihi kwa ajili ya ndugu zangu hasa, wale walio wa kabila langu kwa jinsi ya mwili,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Al-Masihi kwa ajili ya ndugu zangu hasa, wale walio wa kabila langu kwa jinsi ya mwili,

Tazama sura Nakili




Waroma 9:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa.


Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.


Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye khabari zako kutoka Yahudi, wala hapana ndugu hatta mmoja aliyefika hapa na kutupasha khabari, au kunena neno baya juu yako.


khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,


BASSI, nauliza. Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! maana mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila ya Benjamin.


Huenda nikapata kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi vao.


Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumba ya Nakisso, walio katika Kristo.


Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yason, na Sosipatro, jamaa zangu.


Nisalimieni Androniko na Junia; jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, walio maarufu katika mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.


ya kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu.


Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hapana mtu asemae katika Roho ya Mungu, anenae, Yesu ni anathema; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.


Mtu aliye yote asiyempenda Bwana Yesu Kristo, na awe anathema. Maranatha.


Na kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu: ingawa nizidipo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?


Lakini sisi au malaika wa mbinguni tukiwakhubiri ninyi injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.


Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awae yote akiwakhubiri injili illa hiyo tuliyowakhubiri, na alaaniwe.


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.


Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti:


Watumwa, watiini walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili kana kwamba ni kumtii Kristo, kwa khofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo