Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 9:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 ndio sisi tulioitwa nae, si watu wa Wayahudi tu, illa watu wa mataifa pia, utasemaje?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Maana sisi ndio hao aliowaita, si kutoka miongoni mwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Maana sisi ndio hao aliowaita, si kutoka miongoni mwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Maana sisi ndio hao aliowaita, si kutoka miongoni mwa Wayahudi tu bali pia kutoka kwa watu wa mataifa mengine.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Hivi vyombo ni sisi, ambao pia alituita, sio kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 yaani pamoja na sisi, ambao pia alituita, si kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa?

Tazama sura Nakili




Waroma 9:24
20 Marejeleo ya Msalaba  

Simeon ametueleza jinsi Mungu alivyowaangalia mataifa illi achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.


Kwa maana hapana tofanti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri wa kufaa watu wote wamwitiao;


Mungu ni mwaminifu, ambae mliitwa nae muingie katika ushirika wa Mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Akaniambia, Andika, Wa kheri walioitwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo