Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 9:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 tena ajulishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema alivyovitengeneza tangu zamani, vipate utukufu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Alitaka pia kudhihirisha wingi wa utukufu wake ambao alitumiminia sisi tulio lengo la huruma yake; sisi ambao alikwisha kututayarisha kuupokea utukufu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake,

Tazama sura Nakili




Waroma 9:23
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa.


Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba?


Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, illi awe mzaliwa wa kwanza katika ndugu wengi.


Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hawa akawatukuza.


macho ya akili zenu yakitiwa nuru, mjue tumaini la wito wake jinsi lilivyo, na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo,


Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tokea awali illi tuenende nayo.


illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu.


awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho yake, katika mtu wa ndani;


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


mkimshukuru Baba, aliyetustahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru;


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo,


Bassi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hawa atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa killa kazi iliyo njema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo