Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 9:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Lakini, ili Mungu aonekane kwamba anao uhuru wa kuchagua, hata kabla wale ndugu hawajazaliwa na kabla hawajaweza kupambanua jema na baya,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lolote jema au baya, ili kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Lakini, hata kabla hao mapacha hawajazaliwa au kufanya jambo lolote jema au baya, ili kwamba kusudi la Mungu la kuchagua lipate kusimama,

Tazama sura Nakili




Waroma 9:11
22 Marejeleo ya Msalaba  

(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, avitajae vitu visivyokuwa kana kwamba vimekuwa.


ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.


wala si kwa matendo, asije mtu awae yote akajisifu.


kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.


tukijua, ndugu mnaopendwa na Mungu, uteule wenu,


illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.


aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;


alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo