Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 8:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini nyinyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini nyinyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini nyinyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu ambaye hana Roho wa Al-Masihi, huyo si wa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mwenyezi Mungu anakaa ndani yenu. Mtu yeyote ambaye hana Roho wa Al-Masihi, yeye si wa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Waroma 8:9
35 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Baba aliye mbinguni, je! hatazidi na kuwapa wote wamwombao Roho Mtakatifu?


Roho ya kweli; ambae ulimwengu hauwezi kumkubali, kwa kuwa haumwoni wala haumjui: bali ninyi mnamjua; maana anakaa kwenu, nae atakuwa ndani yenu.


Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.


Walipofika kukabili Musia, wakajaribu kwenda Bithunia, lakini Roho ya Yesu hakuwapa rukhusa,


Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja.


Hamjui ya kuwa ninyi hekalu ya Mungu, na ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu?


Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja nae.


Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe;


Je! mnayaangalia yaliyo mbele ya macho yenu? Mtu akijitumainia nafsi yake ya kuwa yeye ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi tu watu wa Kristo.


Kwa maana ninyi hekalu la Mungu aliye hayi; kama Mungu alivyosema, ya kama, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba.


Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.


katika huyo na ninyi, mkiisha kulisikia neno la kweli, khabari njema ya wokofu wenu, katika huyo tena mkiisha kumwamini, mlitiwa muhuri na Roho yule Mtakatifu wa ahadi yake,


katika yeye na ninyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.


Kristo akae mioyoni mwemi kwa imani; illi ninyi, mkiwa na mizizi na misingi katika upendo,


Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokofu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho ya Yesu Kristo,


Ilinde ile amana nzuri kwa Rolio Mtakatifu akaae ndani yetu.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


Nae azishikae amri zake hukaa ndani yake, nae ndani yake. Na hivi tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa Roho aliyotupa.


Hivi tunafahamu ya kuwa tunakaa ndaui yake, nae ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho yake.


Ninyi, watoto wangu, mwatokana na Mungu: nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo