Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 8:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Ni nani atakaewahukumu? Kristo ndiye aliyekufa, naam, na zaidi ya haya, amefufuka, nae yuko mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anaetuombea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka kwa wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka kwa wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka kwa wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Ni nani basi atakayewahukumia adhabu? Hakuna! Al-Masihi Isa aliyekufa, naam, na zaidi ya hayo, akafufuliwa kutoka kwa wafu, yuko mkono wa kuume wa Mungu, naye pia anatuombea.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Ni nani basi atakayewahukumia adhabu? Al-Masihi Isa aliyekufa, naam, zaidi ya hayo, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, yuko mkono wa kuume wa Mungu, naye pia anatuombea.

Tazama sura Nakili




Waroma 8:34
37 Marejeleo ya Msalaba  

kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Bado kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona; kwa sababu mimi ni hayi, ninyi nanyi mtakuwa hayi.


Na siku ile hamtaniuliza neno. Amin, amin, nawaambieni, Mkimwomba Baba neno kwa jina langu atawapeni.


Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha.


Maana Kristo alikufa akafufuka akawa hayi tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hayi pia.


aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Na yeye aichunguzae mioyo aijua nia ya Roho, ya kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.


BASSI mkiwa mmefufuka panioja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko mkono wa kuume wa Mungu, ameketi.


Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;


Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyiku kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu palipo patakatifu khalisi; hali aliingia mbinguni khassa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo