Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 8:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Maana, sheria ya Roho iletayo uhai kwa kuungana na Kristo Yesu imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Maana, sheria ya Roho iletayo uhai kwa kuungana na Kristo Yesu imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Maana, sheria ya Roho iletayo uhai kwa kuungana na Kristo Yesu imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Al-Masihi Isa imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Al-Masihi Isa imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Tazama sura Nakili




Waroma 8:2
29 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.


tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru.


Bassi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.


Nisalimieni Priska na Akula, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,


Ku wapi, bassi, kujisifu? Knmefungiwa mlango. Kwa sharia ya namna gani? Kwa sharia ya matendo? La! bali kwa sharia ya imani.


illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.


Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema.


na mlipokwisha kuandikwa huru mkawa mbali ya dhambi, mlifanywa watumwa wa haki.


Lakini sasa mkiisha kuandikwa huru, na kuwa mbali ya dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, faida yenu mnayo, ndio kutakaswa, na mwisho wake uzima wa milele.


Bassi nimeona sharia hii ya kuwa nipendapo kutenda lililo jema, liapo lililo baya ni karibu nami.


lakini katika viungo vyangu naona sharia nyingine inapiga vita na ile sharia ya akili zangu, na kunifanya mateka va ile sharia ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.


Kadhalika, ndugu zangu, na ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka, kusudi tumzalie Mungu matunda.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza Adamu alikuwa nafsi hayi; Adamu wa mwisho roho yenye kuhuisha.


Bassi Bwana ndiye Roho huyo; walakini alipo Roho ya Bwana, hapo ndipo panapo uhuru.


aliyetutosheleza kuwa wakhudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha.


Maana mimi kwa sharia naliifia sharia illi nimwishie Mungu.


KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.


Mchukuliane mizigo mkaitimize hivyo sharia ya Kristo.


Lakini aliyeitazama sharia kamilifu ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyu atakuwa wa kheri katika kutenda kwake.


Na baada ya siku tatu u nussu roho ya uhayi itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama, khofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo