Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 8:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Kwa kuwa hamkupokea roho ya utumwa uletao khofu, hali mlipokea roho ya kufanywa waua, kwa hiyo twalia, Abba, Baba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kwa maana, hamkumpokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watumwa tena na kuwatia hofu, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watoto wa Mungu, na kwa Roho huyo, sisi tunamwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kwa maana, hamkumpokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watumwa tena na kuwatia hofu, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watoto wa Mungu, na kwa Roho huyo, sisi tunamwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kwa maana, hamkumpokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watumwa tena na kuwatia hofu, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watoto wa Mungu, na kwa Roho huyo, sisi tunamwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu tena, bali mlipokea Roho wa kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, “Abba, Baba.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iwaleteayo tena hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, “Abba, yaani, Baba.”

Tazama sura Nakili




Waroma 8:15
30 Marejeleo ya Msalaba  

nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako chini ya inchi: tazama, unayo iliyo yako.


Akasema, Abba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikomhe hiki: walakini, si nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.


Akawaambia, Msalipo, semeni: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako takatifu litukuzwe.


Baba, ukipenda, uniondolee kikombe hiki: lakini si kama nitakavyo mimi, illa utakavyo wewe vifanyike.


Alipomwona Yesu, akapiga kelele, akamwangukia, akasema kwa sauti kuu. Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuomba usiniadhibu.


Na watu wote wa inchi ya Wagadarene iliyo kando kando wakamwomba aondoke kwao, kwa sababu walishikwa na khofu nyingi; bassi akakiingia chombo akarudi.


Na akiisha kuja yeye, atauhakikisha ulimwengu kwa khabari ya dhambi, na haki, na hukumu;


Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.


Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa khofu, akawaangukia miguu Paolo na Sila;


Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?


Roho yenyewe hushuhudu pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;


Wala si hivyo tu, illa na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho tunaugua katika nafsi zetu, tukitazamia kufanywa wana, ukombozi wa mwili wetu.


Na kadhalika Roho nae hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuomhea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.


ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao,


Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu.


Maana yeye ajae akikhubiri Yesu mwingine ambae sisi hatukumkhubiri, au mkipokea Roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumilia nae.


bali kwa ajili ya ndugu za uwongo walioingizwa kwa siri.


KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.


Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,


Maana Mungu hakutupa roho ya khofu, bali ya nguvu na ya upendo ua ya moyo wa kiasi.


akawaokoe wale ambao kwamba maisha zao zote kwa khofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.


Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vyema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.


Katika pendo hamua khofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje khofu, kwa maana khofu ina adhabu; na mwenye khofu hakukamilishwa katika pendo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo