Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 8:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Isa kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Al-Masihi Isa kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kupitia kwa Roho wake Mtakatifu akaaye ndani yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Nanyi ikiwa Roho wa Mwenyezi Mungu aliyemfufua Isa kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Al-Masihi Isa kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.

Tazama sura Nakili




Waroma 8:11
37 Marejeleo ya Msalaba  

Roho ya kweli; ambae ulimwengu hauwezi kumkubali, kwa kuwa haumwoni wala haumjui: bali ninyi mnamjua; maana anakaa kwenu, nae atakuwa ndani yenu.


Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao.


Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Nisalimieni Apelle, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumba ya Aristobulo.


Nisalimieni Priska na Akula, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,


Nisalimieni Androniko na Junia; jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, walio maarufu katika mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.


Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Staku, mpenzi wangu.


Bassi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hatta mkazitii tamaa zake;


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Bassi, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.


Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo nae hakufufuliwa.


Na Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua na sisi kwa uweza wake.


Maana sisi tulio hayi siku zote twatolewa tufe kwa ajili ya Yesu, illi uzima wa Yesu udhihirishwe katika miili yetu ipatwayo na manti.


tukijua kama yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi.


Kwa maana sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, hali kuvikwa vazi jingine, illi kitu kile kipatwacho na mauti kimezwe na uzima.


Maana yeye apandae kwa mwili wake, katika mwili atavuna uharibifu; bali yeye apandae kwa Roho, katika Roho atavima uzima wa milele.


hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema);


atakaeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule awezao kuvitiisha hatta na vitu vyote chini yake.


Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Na baada ya siku tatu u nussu roho ya uhayi itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama, khofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo