Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 7:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Tusemeje, bassi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalijua dhambi illa kwa sharia: kwa maana singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Je, tuseme basi, kwamba sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakini bila sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani. Maana, nisingalijua ni nini hasa kutamani mabaya, kama sheria isingalikuwa imesema: “Usitamani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Je, tuseme basi, kwamba sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakini bila sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani. Maana, nisingalijua ni nini hasa kutamani mabaya, kama sheria isingalikuwa imesema: “Usitamani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Je, tuseme basi, kwamba sheria ni dhambi? Hata kidogo! Lakini bila sheria, mimi nisingalijua dhambi ni kitu gani. Maana, nisingalijua ni nini hasa kutamani mabaya, kama sheria isingalikuwa imesema: “Usitamani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Tuseme nini basi? Kwamba Torati ni dhambi? La, hasha! Lakini singejua dhambi isipokuwa kwa sababu ya Torati. Singejua kutamani ni nini kama Torati haikusema, “Usitamani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Tuseme nini basi? Kwamba Torati ni dhambi? La, hasha! Lakini, isingekuwa kwa sababu ya Torati, nisingalijua dhambi. Nisingalijua kutamani ni nini kama Torati haikusema, “Usitamani.”

Tazama sura Nakili




Waroma 7:7
30 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mimi miwaambieni, Killa mtu atazamae mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini nae moyoni mwake.


Akawaambia, Angalieni, jilindeni na kutamani, maana uzima wa mtu hautoki katika mali zake, kwa sababu ana wingi wa mali.


Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.


Sikutamani fedha, wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.


Maana ile, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishududu uwongo, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani wako kama nafsi yako.


kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.


Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.)


BASSI, tusemeje? Ibrahimu baba yetu kwa jinsi ya mwili amepata nini?


Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa.


Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


Ni nini bassi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sharia bali chini ya neema? Hasha!


Kwa maana dhambi, ikipata nafasi kwa iie amri, ilinidanganya, ikaniua kwayo.


Bassi je! Ile iliyo njema ilikuwa manti kwangu mimi? Hasha! hali dhambi, illi ionekane kuwa dhambi, ilinifanyizia mauti kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.


Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao.


Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanza ndani yangu killa namna ya tamaa. Kwa maana dhambi hila sharia ni kifu.


Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni sharia.


Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu;


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu;


(kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo