Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 7:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Maana, tulipokuwa tukiishi kimaumbile tu, tamaa mbaya zikichochewa na sheria, zilifanya kazi katika miili yetu, na kuchuma pato la kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Maana, tulipokuwa tukiishi kimaumbile tu, tamaa mbaya zikichochewa na sheria, zilifanya kazi katika miili yetu, na kuchuma pato la kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Maana, tulipokuwa tukiishi kimaumbile tu, tamaa mbaya zikichochewa na sheria, zilifanya kazi katika miili yetu, na kuchuma pato la kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kwa maana tulipokuwa tunatawaliwa na asili ya dhambi, tamaa za dhambi zilizochochewa na Torati zilikuwa zikitenda kazi katika miili yetu, hivyo tulizaa matunda ya mauti.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwa maana tulipokuwa tunatawaliwa na asili ya dhambi, tamaa za dhambi zilizochochewa na Torati zilikuwa zikitenda kazi katika miili yetu, hivyo tulizaa matunda ya mauti.

Tazama sura Nakili




Waroma 7:5
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, mauaji, mazini, asharati, uizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano;


Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.


Kwa hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hatta wanawake wakahadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili:


kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.


Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa.


Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


wala msitoe viungo vyenu kuwa silaha ya dhulumu kwa dhambi; bali jitoeni nafsi zenu sadaka kwa Mungu kama walio hayi baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.


Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa maana kama mlivyotoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na maasi mpate kuasi, vivyo sasa toeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.


Faida gani bassi mliyopata siku zile kwa mambo haya mnayotahayarikia sasa? kwa maana mwisho wa mambo haya ni mauti.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


lakini katika viungo vyangu naona sharia nyingine inapiga vita na ile sharia ya akili zangu, na kunifanya mateka va ile sharia ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.


Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni sharia.


Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.


Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.


Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono:


ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.


Bassi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika inchi, uasharati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu:


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Khalafu ile tamaa ikiisha kuchuikua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.


VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?


Killa afanyae dhambi, afanya nasi; kwa kuwa dhambi ni nasi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo