Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 7:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Kadhalika, ndugu zangu, na ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka, kusudi tumzalie Mungu matunda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Hali kadhalika nyinyi ndugu zangu: Nyinyi pia mmekufa kuhusu sheria kwa kuwa nyinyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Hali kadhalika nyinyi ndugu zangu: Nyinyi pia mmekufa kuhusu sheria kwa kuwa nyinyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Hali kadhalika nyinyi ndugu zangu: nyinyi pia mmekufa kuhusu sheria kwa kuwa nyinyi ni sehemu ya mwili wa Kristo; sasa mmekuwa wake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu ili tupate kuzaa matunda mema kwa ajili ya Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia Torati kupitia kwa mwili wa Al-Masihi, ili mweze kuwa mali ya mwingine, yeye ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu, ili tupate kuzaa matunda kwa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Vivyo hivyo, ndugu zangu, ninyi mmeifia Torati kwa njia ya mwili wa Al-Masihi, ili mweze kuwa mali ya mwingine, yeye ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu, ili tupate kuzaa matunda kwa Mungu.

Tazama sura Nakili




Waroma 7:4
35 Marejeleo ya Msalaba  

Walipokuwa wakila, Yesu akatwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ni mwili wangu.


Na hawa ndio waliopandwa panapo udongo mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, moja thelathini, moja sittini, na moja mia.


Kwa hiyo atukuzwa Baba yangu, mzae sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.


Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia.


Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.


Vivyo hivyo na ninyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na wahayi kwa Mungu katika Kristo Yesu.


Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema.


Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?


Lakini sasa mkiisha kuandikwa huru, na kuwa mbali ya dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, faida yenu mnayo, ndio kutakaswa, na mwisho wake uzima wa milele.


Bassi wakati awapo hayi mume wake, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Bali mume wake akifa, amekuwa huru, hafungwi na sharia hiyo, hatta yeye si mzinzi, ajapokuwa na mume mwingine.


Bali sasa tumetolewa katika torati isitukhusu kitu, tumeilia hali ile iliyotupinga, tupate kutumika sisi katika hali mpya chini ya roho, si katika hali ya zamani, ya dini ya sharia iliyoandikwa.


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule timmegao, si ushirika wa mwili wti Kristo?


Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; maana naliwaposea mume mmoja, nimletee Kristo bikira safi.


Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti:


Lakini nikiongozwa na Roho, hunpo chini ya sharia.


akiisha kuuondoa kwa mwili wake ule uadui, ndio sharia ya amri zilizo katika maagizo; illi afanye wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake, akifanya amani;


mmejazwa matuuda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.


Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.


mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; kwa killa kazi njema mkizaa matunda, mkizidi katika maarifa ya Mungu;


katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


akiisba kuifuta ile khati iliyoandikwa na kutushitaki kwa hukumu zake; iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwe kati kati yetu sisi na yeye, akaikaza msalabani;


Bassi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkaacha mafundisho ya awali ya ulimwengu, ya nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani,


Katika mapenzi hayo tumepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo marra moja.


yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, illi, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe bayi kwa mambo ya haki; kwa kuchubuka kwake mliponywa.


Na tufurahi tukashangilie tukampe ulukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.


Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo