Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 7:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Ole wangu mimi bin Adamu! nani atakaeniokoa na mwili huu wenye kunifisha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka mwili huu unaonipeleka kifoni?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka mwili huu unaonipeleka kifoni?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Maskini miye! Nani atakayeniokoa kutoka mwili huu unaonipeleka kifoni?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Ole wangu, mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

Tazama sura Nakili




Waroma 7:24
36 Marejeleo ya Msalaba  

Wa kheri wenye huzuni: maana hawo watafarajika.


Wa kheri wenye njaa na kiu ya haki: maana hawo watashiba.


Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa,


tukijua haya, ya kuwa mtu wetu wa kale alisulibishwa pamoja nae, illi mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;


kwa maana kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa: bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Wala si hivyo tu, illa na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho tunaugua katika nafsi zetu, tukitazamia kufanywa wana, ukombozi wa mwili wetu.


Na kadhalika Roho nae hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuomhea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.


Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mkono, kwa kuuvua mwili wa dhambi, wa nyama, kwa tohara ya Kristo;


Na Bwana ataniokoa na killa neno baya na kunihifadhi hatta uje ufalme wake wa milele.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


akawaokoe wale ambao kwamba maisha zao zote kwa khofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.


Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo