Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 7:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai neno jema: kwa kuwa kutaka ni katika uwezo wangu, bali kutenda lililo jema sipati.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi kulitekeleza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi kulitekeleza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Najua kwamba hamna jema lolote ndani yangu mimi, kadiri ya ubinadamu wangu. Kwa maana, ingawa nataka kufanya jambo jema, siwezi kulitekeleza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote linalokaa ndani yangu, yaani katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda.

Tazama sura Nakili




Waroma 7:18
31 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, mauaji, mazini, asharati, uizi, ushuhuda wa uwongo, na matukano;


Bassi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Baba aliye mbinguni, je! hatazidi na kuwapa wote wamwombao Roho Mtakatifu?


Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.


Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msitafakari mahitaji ya mwili, nisije mkawasha tamaa zake.


Maana sijui nifanyalo; kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; na lile nilichukialo nalitenda.


Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi, bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.


Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Bassi, kama ni hivi, kwa akili zangu naitumikia sharia ya Mungu, bali kwa mwili sharia ya dhambi.


Kwa maana tulipokuwa katika mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati zilitenda (kazi) katika viungo vyetu hatta tukaizalia mauti mazao.


Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana liizi zimepingana, hatta hamwezi kufanya nmayotaka.


Nao walio watu wa Kristo Yesu wameusulibisha niwili pamoja na mawazo mabaya na tamaa mbaya.


kwa maana ni Mungu atendae ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa ajili ya kusudi lake jema.


Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! bali nafuatafuata illi nilishike lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


kuanzia sasa tusiendelee kuishi katika tamaa za wana Adamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wetu wa kukaa hapa duniani uliobakia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo