Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 6:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Yesu Kristo, twalibatizwa katika mauti yake?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Maana, mnajua kwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Maana, mnajua kwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Maana, mnajua kwamba sisi tuliobatizwa tukaungana na Kristo Yesu, tulibatizwa na kuungana na kifo chake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Al-Masihi Isa tulibatizwa katika mauti yake?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Al-Masihi Isa tulibatizwa katika mauti yake?

Tazama sura Nakili




Waroma 6:3
24 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Waliposikia baya wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


kwa maana bado hajawashukia hatta mmoja wao, illa wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.


Hamjui ya kuwa kwake yeye ambae mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake na kumtumikia, m watumwa wake yule mmtiiye, ikiwa utumishi wa dhambi uletao mauti, au utumishi wa utii uletao haki.


Lakini tukiwa twalikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja nae,


HAMJUI, ndugu (maana nasema nao waijuao sharia), ya kuwa torati humtawala mtu maadam yu hayi.


wote wakabatizwa kwa Musa katika wingu na katika bahari;


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje, bassi, kama wafu hawafufuki?


Hamjui ya kuwa ninyi hekalu ya Mungu, na ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa ndani yenu?


Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulitia chachu donge zima?


Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu ya Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyopewa na Mungu? Na ninyi si mali yenu wenyewe;


Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike. Waasharati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa kike, wala wafira,


Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula sehemu ya vitu vya hekalu, na wale waikhudumiao madhbahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhbahu?


Hamjui, ya kuwa washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeao tunzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, illi mpate.


Jijaribuni nafsi zenu kwamba m katika imani; jithubutisheni nafsi zenu. Au bamjijui nafsi zenu, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu isipokuwa mmekataliwa?


Maana ninyi nyote mliobatizwa na kuingizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.


Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo