Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 6:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Maana, dhambi haitawatawala tena, kwani hamko chini ya sheria, bali chini ya neema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Maana, dhambi haitawatawala tena, kwani hamko chini ya sheria, bali chini ya neema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Maana, dhambi haitawatawala tena, kwani hamko chini ya sheria, bali chini ya neema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.

Tazama sura Nakili




Waroma 6:14
25 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atazaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, ndiye atakaewaokoa watu wake na dhambi zao.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Bassi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.


Lakini ikiwa ni kwa neema yake, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema; na ikiwa ni kwa matendo, haiwi neema tena, au hapo matendo yasingekuwa matendo.


Kwa hiyo ilitoka kwa imani, iwe kwa njia ya neema, illi ile ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa torati tu, illa na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote,


Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.


Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima.


Bassi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hatta mkazitii tamaa zake;


Ni nini bassi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sharia bali chini ya neema? Hasha!


Bassi, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Lakini kabla ya kuja imani tulikuwa tumewekwa chini ya sharia, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.


Niambieni, ninyi ninaotaka kuwa chini ya sharia, hamwisikii torati?


Lakini nikiongozwa na Roho, hunpo chini ya sharia.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo