Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 5:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepcwa sisi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha mimina mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha mimina mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha mimina mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kupitia kwa Roho wa Mungu ambaye ametupatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho wa Mwenyezi Mungu ambaye ametupatia.

Tazama sura Nakili




Waroma 5:5
35 Marejeleo ya Msalaba  

Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.


Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto:


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu: Neema iwe kwenu na imani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwaua Yesu Kristo.


Na twajua ya kuwa mambo yote hushiriki kazi moja, ndio kuwapatia mema wale wampendao Mungu, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.


kama ilivyoandikwa, Tazama, Naweka katika Sayuni jiwe likwaazalo, na mwamba uangushao: Na killa amwaminiye hataaibishwa.


Lakini mtu akimpenda Mungu, huyo amejuliwa nae.


nae ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.


Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amin.


Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.


Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.


Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


katika huyo na ninyi, mkiisha kulisikia neno la kweli, khabari njema ya wokofu wenu, katika huyo tena mkiisha kumwamini, mlitiwa muhuri na Roho yule Mtakatifu wa ahadi yake,


Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.


kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.


Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.


Na Bwana wetu Yesu Kristo, na Mungu Baba yetu aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema,


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


Sisi twapenda kwa maana yeye kwanza alitupenda sisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo