Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 5:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Kama vile dhambi ilivyotawala kwa kifo, kadhalika neema inatawala kwa uadilifu na kuleta uhai wa milele kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Kama vile dhambi ilivyotawala kwa kifo, kadhalika neema inatawala kwa uadilifu na kuleta uhai wa milele kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Kama vile dhambi ilivyotawala kwa kifo, kadhalika neema inatawala kwa uadilifu na kuleta uhai wa milele kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 ili kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo neema iweze kutawala kupitia kwa haki hata kuleta uzima wa milele katika Isa Al-Masihi Bwana wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala kwa njia ya mauti, vivyo hivyo neema iweze kutawala kwa njia ya kuhesabiwa haki hata kuleta uzima wa milele katika Isa Al-Masihi Bwana wetu.

Tazama sura Nakili




Waroma 5:21
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu.


Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sharia bali kwa wema aliopata kwa imani.


Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote;


lakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hatta wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu aliye mfano wake yeye atakaekuja.


Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.


Bassi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hatta mkazitii tamaa zake;


Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema.


Hamjui ya kuwa kwake yeye ambae mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake na kumtumikia, m watumwa wake yule mmtiiye, ikiwa utumishi wa dhambi uletao mauti, au utumishi wa utii uletao haki.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu u katika hali ya kufa kwa sababu ya dhambi, bali roho yenu i katika hali ya uzima, kwa sababu ya haki.


Maana neema ya Mungu iwaokoayo wana Adamu wote imeonekana;


Bassi na tukikaribie kiti cha neema kwa nthubuitifu, illi tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo