Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 5:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wote waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwake mtu mmoja watu wote wameingizwa katika hali ya wenye haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Na kama kwa kutokutii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi, kadhalika kutii kwa mtu mmoja kutawafanya wengi kuwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Na kama kwa kutokutii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi, kadhalika kutii kwa mtu mmoja kutawafanya wengi kuwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Na kama kwa kutokutii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi, kadhalika kutii kwa mtu mmoja kutawafanya wengi kuwa waadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Kwa maana kama vile kupitia kutokutii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kupitia kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Kwa maana kama vile kwa kutokutii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki.

Tazama sura Nakili




Waroma 5:19
10 Marejeleo ya Msalaba  

Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi illi awarehemu wote.


Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote;


Lakini kipawa kile hakikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kuanguka kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema ya mtu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.


Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima.


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:


tena, alipoonekana ana umho kama mwana Adamu, alijidhili, akawa mtii hatta mauti, nayo mauti ya msalaba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo