Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 5:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Bassi tena, kama vile kwa anguko moja watu wote walihukumiwa, vivyo hivyo kwa tendo moja la haki watu wote walipewa haki yenye uzima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kiadilifu cha mtu mmoja kinawapa wote uadilifu na uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kiadilifu cha mtu mmoja kinawapa wote uadilifu na uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kiadilifu cha mtu mmoja kinawapa wote uadilifu na uhai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la haki la mtu mmoja lilileta kuhesabiwa haki ambako huleta uzima kwa wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa hiyo, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la haki la mtu mmoja lilileta kuhesabiwa haki ambako huleta uzima kwa wote.

Tazama sura Nakili




Waroma 5:18
17 Marejeleo ya Msalaba  

Huyu alikuja kwa ushuhuda, illi aishuhudie nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.


Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu.


Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabbi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ngʼambu ya Yardani, uliyemshuhudia wewe, huyu nae anabatiza, na watu wote wanamwendea.


na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa.


ambae Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa damu yake, kwa njia ya imani, illi aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizotangulia, katika uvumilivu wa Mungu:


aliyetolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa illi tupate kupewa haki.


Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote;


Lakini kipawa kile hakikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kuanguka kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema ya mtu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.


Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wote waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwake mtu mmoja watu wote wameingizwa katika hali ya wenye haki.


Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema.


Kwa kuwa katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.


illa twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, illi kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya killa mtu.


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo