Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 5:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Kweli, kwa dhambi ya mtu mmoja, kifo kilianza kutawala kwa sababu ya huyo mtu mmoja; lakini, ni dhahiri zaidi kwamba alichokifanya yule mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, ni bora zaidi. Wote wanaopokea neema na zawadi hiyo ya kufanywa kuwa waadilifu, watatawala katika uhai kwa njia ya huyo mmoja, yaani Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Kweli, kwa dhambi ya mtu mmoja, kifo kilianza kutawala kwa sababu ya huyo mtu mmoja; lakini, ni dhahiri zaidi kwamba alichokifanya yule mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, ni bora zaidi. Wote wanaopokea neema na zawadi hiyo ya kufanywa kuwa waadilifu, watatawala katika uhai kwa njia ya huyo mmoja, yaani Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Kweli, kwa dhambi ya mtu mmoja, kifo kilianza kutawala kwa sababu ya huyo mtu mmoja; lakini, ni dhahiri zaidi kwamba alichokifanya yule mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, ni bora zaidi. Wote wanaopokea neema na zawadi hiyo ya kufanywa kuwa waadilifu, watatawala katika uhai kwa njia ya huyo mmoja, yaani Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kupitia kwa huyo mtu mmoja, yaani Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mtu mmoja, yaani, Isa Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Waroma 5:17
26 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


Mwizi haji illa aibe, achinje, aharibu; mimi nalikuja wawe na uzima, na wawe nao tele.


Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote;


Lakini kipawa kile hakikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kuanguka kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema ya mtu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.


Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sharia, hali chini ya neema.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe cho chote kinginecho hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Yesu Kristo Bwana wetu.


Na kama tulivyoichukua sura yake wa udongo, kadhalika tulaichukua sura yake wa mbinguni.


Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Na ingekuwa kheri kama mngalimiliki, illi sisi nasi tumiliki pamoja nanyi.


tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;


na neema ya Bwana wetu ilizidi sana pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.


Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo