Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 5:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyekosa si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu, bali kipawa cha neema kilikuja kwa ajili ya makosa mengi, kikaleta kuachiliwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu na dhambi ya mtu yule mmoja. Maana, baada ya kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu; lakini baada ya makosa ya watu wengi, Mungu aliwapa zawadi yake kwa kuwasamehe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu na dhambi ya mtu yule mmoja. Maana, baada ya kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu; lakini baada ya makosa ya watu wengi, Mungu aliwapa zawadi yake kwa kuwasamehe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu na dhambi ya mtu yule mmoja. Maana, baada ya kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu; lakini baada ya makosa ya watu wengi, Mungu aliwapa zawadi yake kwa kuwasamehe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Tena ile karama ya Mungu haiwezi kulinganishwa na matokeo ya ile dhambi ya mtu mmoja. Kwani hukumu ilikuja kupitia kwa dhambi ya mtu mmoja, ikaleta adhabu; lakini ile karama ilikuja baada ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Tena, ile karama ya Mungu si kama matokeo ya ile dhambi. Hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja, ikaleta adhabu, bali karama ya neema ya Mungu ilikuja kwa njia ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki.

Tazama sura Nakili

Waroma 5:16
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa wako ni ufalme, na nguvu, na utukufu, hatta milele. Amin. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe nanyi.

SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.

Tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, tusipate kupasishwa adhabu pamoja na dunia.

Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.

Maana mtu awae yote atakaeishika sharia yote, na pamoja na hayo, akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo