Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 4:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Bassi ukheri huu ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba Ibrahimu kwa ajili ya imani yake aliliesabiwa wema.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Je, hiyo ni kwa wale waliotahiriwa tu, ama pia kwa wale wasiotahiriwa? Ni kwa wale wasiotahiriwa pia. Kwa maana tumekwisha sema: “Abrahamu aliamini, naye Mungu akamkubali kuwa mwadilifu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Je, huku kubarikiwa ni kwa wale waliotahiriwa peke yao, au pia na kwa wale wasiotahiriwa? Tumesema imani ya Ibrahimu ilihesabiwa kwake kuwa haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Je, huku kubarikiwa ni kwa wale waliotahiriwa peke yao, au pia na kwa wale wasiotahiriwa? Tunasema, “Imani ya Ibrahimu ilihesabiwa kwake kuwa haki.”

Tazama sura Nakili

Waroma 4:9
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.

Alihesabiwaje bassi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.

Maana maandiko yasemaje? Ibrabimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

illi baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupewa ahadi ya Roho kwa njia ya imani.

Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;

Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo