Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 4:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Lakini kwa mtu asiofanya kazi, bali anamwammi yeye ampae haki asiye mtawa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Lakini mtu asiyetegemea matendo yake mwenyewe, bali anamwamini Mungu ambaye huwasamehe waovu, basi, Mungu huijali imani ya mtu huyo, akamkubali kuwa mwadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Lakini mtu asiyetegemea matendo yake mwenyewe, bali anamwamini Mungu ambaye huwasamehe waovu, basi, Mungu huijali imani ya mtu huyo, akamkubali kuwa mwadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Lakini mtu asiyetegemea matendo yake mwenyewe, bali anamwamini Mungu ambaye huwasamehe waovu, basi, Mungu huijali imani ya mtu huyo, akamkubali kuwa mwadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Lakini kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, yeye ambaye huwahesabia waovu haki, imani yake inahesabiwa kuwa haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Lakini kwa mtu ambaye hafanyi kazi na anamtumaini Mungu, yeye ambaye huwahesabia waovu haki, imani yake inahesabiwa kuwa haki.

Tazama sura Nakili

Waroma 4:5
24 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Ukiweza kuamini: yote yawezekana kwake aaminiye.

Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.

Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae.

Kwa maana, wakiwa hawajui haki ya Mungu, na wakitaka kuithubutisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.

ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.

bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu katika wafu, Bwana wetu,

Maana maandiko yasemaje? Ibrabimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

Kama vile Daud aunenavyo ukheri wake mtu yule ambae Mungu amhesabia kuwa na haki pasipo matendo;

tena nionekane katika yeye, nisiwe na baki ile ipatikanayo kwa sharia, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo