Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 4:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Ambae aliamini kwa kutazamia yasiyoweza kutazamiwa, kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa nzao wako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Wazawa wako watakuwa wengi kama nyota!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Wazawa wako watakuwa wengi kama nyota!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Abrahamu aliamini na kutumaini ingawa hali yenyewe ilikuwa bila matumaini, na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Wazawa wako watakuwa wengi kama nyota!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Ibrahimu akaamini, akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyoahidiwa kwamba, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Akitarajia yasiyoweza kutarajiwa, Ibrahimu akaamini, akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyoahidiwa kwamba, “Uzao wako utakuwa mwingi mno.”

Tazama sura Nakili

Waroma 4:18
12 Marejeleo ya Msalaba  

Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje hayo? Maana mimi mzee na mke wangu kongwe wa siku nyingi.

Bassi, wanaume, changaʼmkani; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.

(kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, avitajae vitu visivyokuwa kana kwamba vimekuwa.

Asiyekuwa dhaifu wa imani, wala hakutia moyoni hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa (akiwa amekwisha kupata miaka mia), wala hali ya kufa ya tumbo lake Sara.

na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepcwa sisi.

Kwa maana tuliokolewa kwa kutumaini; lakini kitu kilichotumainiwa kikionekana hakuna kutumaini tena. Kwa maana kile akionacho mtu, ya nini kukitumaini?

tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo mle mlimo ndani ya pazia,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo