Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 4:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi) mbele zake aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, avitajae vitu visivyokuwa kana kwamba vimekuwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.” Ahadi hiyo ni kweli mbele ya Mungu ambaye Abrahamu alimwamini-Mungu ambaye huwapa wafu uhai, na kwa amri yake, vitu ambavyo havikuwapo huwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.” Ahadi hiyo ni kweli mbele ya Mungu ambaye Abrahamu alimwamini-Mungu ambaye huwapa wafu uhai, na kwa amri yake, vitu ambavyo havikuwapo huwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.” Ahadi hiyo ni kweli mbele ya Mungu ambaye Abrahamu alimwamini-Mungu ambaye huwapa wafu uhai, na kwa amri yake, vitu ambavyo havikuwapo huwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu, ambaye yeye alimwamini, yule Mungu anayefufua waliokufa, na kuvitaja vitu ambavyo haviko kana kwamba viko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu, ambaye yeye alimwamini, yule Mungu anaye fufua waliokufa, na kuvitaja vile vitu ambavyo haviko kana kwamba vimekwisha kuwako.

Tazama sura Nakili




Waroma 4:17
32 Marejeleo ya Msalaba  

msiwaze moyoni kwamba, Tuna baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni ya kwamba Mungu anaweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.


Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao.


Amin, amin, nawaambieni, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hayi.


Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.


Kazi zake zote zimejulika na Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu.


Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa mataifa pia? Naam, wa mataifa pia;


Ambae aliamini kwa kutazamia yasiyoweza kutazamiwa, kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa nzao wako.


Kwa maana ikiwa Ibrahimu alipewa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia, lakini si mbele za Mungu.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,


Na itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, Hapo watakwitwa wana wa Mungu aliye hayi.


nae alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, na vitu ambavyo haviko, illi avibatilishe vilivyoko;


Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza Adamu alikuwa nafsi hayi; Adamu wa mwisho roho yenye kuhuisha.


Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,


Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, nae kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufukoni, usioweza kuhesabiwa.


Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hatta vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.


Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu kama siku moja.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo