Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 4:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Kwa hiyo ilitoka kwa imani, iwe kwa njia ya neema, illi ile ahadi iwe imara kwa wazao wote, si kwa wale wa torati tu, illa na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote: Si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali pia kwa wale waishio kwa imani kama Abrahamu. Yeye ni baba yetu sisi sote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote: Si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali pia kwa wale waishio kwa imani kama Abrahamu. Yeye ni baba yetu sisi sote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote: si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali pia kwa wale waishio kwa imani kama Abrahamu. Yeye ni baba yetu sisi sote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kwa hiyo, ahadi huja kupitia kwa imani, ili iwe ni kwa neema, na ihakikishiwe wazao wote wa Ibrahimu, si kwa wale walio wa sheria peke yao, bali pia kwa wale walio wa imani ya Ibrahimu. Yeye ndiye baba yetu sisi sote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwa hiyo, ahadi huja kwa njia ya imani, ili iwe ni kwa neema, na itolewe kwa wazao wa Ibrahimu, si kwa wale walio wa sheria peke yao, bali pia kwa wale walio wa imani ya Ibrahimu. Yeye ndiye baba yetu sisi sote.

Tazama sura Nakili




Waroma 4:16
18 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Leo wokofu umefika nyumbani humu, kwa kuwa huyu nae ni mwana wa Ibrahimu.


Bassi nasema, Yesu Kristo amefanyika mkhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithubutishe ahadi walizopewa haha zetu;


ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.


kama tukijali kwamba Mungu ni mmoja, atakaewapa wale waliotahiriwa haki itokayo katika imani, nao wasiotahiriwa liaki kwa njia ya imani hiyo hiyo.


Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema;


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanabesabiwa kuwa wazao.


illi baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupewa ahadi ya Roho kwa njia ya imani.


Ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa uzao, kana kwamba ni watu wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani Kristo.


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema);


Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu:


tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo