Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waroma 4:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sharia bali kwa wema aliopata kwa imani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mungu alimwahidi Abrahamu na wazawa wake kwamba ulimwengu ungekuwa mali yao. Ahadi hiyo haikufanywa kwa sababu Abrahamu aliitii sheria, bali kwa kuwa aliamini, akakubaliwa kuwa mwadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mungu alimwahidi Abrahamu na wazawa wake kwamba ulimwengu ungekuwa mali yao. Ahadi hiyo haikufanywa kwa sababu Abrahamu aliitii sheria, bali kwa kuwa aliamini, akakubaliwa kuwa mwadilifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mungu alimwahidi Abrahamu na wazawa wake kwamba ulimwengu ungekuwa mali yao. Ahadi hiyo haikufanywa kwa sababu Abrahamu aliitii sheria, bali kwa kuwa aliamini, akakubaliwa kuwa mwadilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa maana ile ahadi kwamba angeurithi ulimwengu haikuja kwa Ibrahimu au kwa wazao wake kupitia kwa sheria bali kupitia kwa haki ipatikanayo kwa imani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa maana ile ahadi kwamba angeurithi ulimwengu haikuja kwa Ibrahimu au kwa wazao wake kwa njia ya sheria bali kwa njia ya haki ipatikanayo kwa imani.

Tazama sura Nakili

Waroma 4:13
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na sisi tunawakhubirieni ahadi ile waliyopewa baba zetu, ya kwamba Mungu ametutimizia sisi watoto wao ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu:

na baba ya kutahiriwa, si kwa hao waliotahiriwa tu, bali kwa hao waliotahiriwa na kuzifuasa uyayo za imani yake baba yetu Ibrahimu aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa.

yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanabesabiwa kuwa wazao.

Na kama ninyi ni wa Kristo, bassi, nimekuwa mzao wa Ibrahimu, na wrarithi kwa ahadi.

Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.

Bali yeye, ambae uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo