Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waroma 3:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Ni nini bassi? Tu bora kuliko wengine? Hatta kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba wote pia wa chini ya dhambi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Tuseme nini, basi? Je, sisi Wayahudi ni bora kuliko wengine? Hata kidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapo mwanzoni kwamba Wayahudi na watu wa mataifa mengine wote wako chini ya utawala wa dhambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Tuseme nini, basi? Je, sisi Wayahudi ni bora kuliko wengine? Hata kidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapo mwanzoni kwamba Wayahudi na watu wa mataifa mengine wote wako chini ya utawala wa dhambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Tuseme nini, basi? Je, sisi Wayahudi ni bora kuliko wengine? Hata kidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapo mwanzoni kwamba Wayahudi na watu wa mataifa mengine wote wako chini ya utawala wa dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Tusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi.

Tazama sura Nakili




Waroma 3:9
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.


Kwa maana ghadhahu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wana Adamu waipingao kweli kwa uovu wao.


Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi illi awarehemu wote.


Imekuwaje bassi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata, lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu.


KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.


BASSI Myahudi ana ziada gani? na kutahiriwa kwafaa nini?


Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithubutisha hakiya Mungu, tuseme nini? Mungu ni dhalimu aletae ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibin-Adamu.)


Ni nini bassi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sharia bali chini ya neema? Hasha!


Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni, bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.


Bassi niseme nini? ya kwamba sanamu ni kitu? au ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?


Imekuwaje, bassi? Nitaomba kwa roho, na nitaomba kwa akili; nitaimba kwa roho, na nitaimba kwa akili.


Maana ni nani anaekupambanua na mwingine? na una, nini usiyoipokea? Na iwapo uliipokea, wajisifiani kana kwamba hukuipokea?


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


Yadhuru nini? bali kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anakhubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo